...

3 views

MPENZI ,, ,,
Najitoa kwenye baridi,
kwa ajili yako ua ridi,
japo nafahamu ya wambea,
nitasalia kwako kubembea ,
penzi letu na litie nanga,
tusalie kuwa mwanga.

Naomba kukulea,
mapenzi yanavyo zidi kukolea,
ya umbo nisije kuzungumzia
mafisi wakakufukuzia
Kate usiwe kama vibanzi,
ukaliwa nijitie kitanzi.

Sisemi kwa kulalama ,
isije kunitia lawama ,
wewe ndiwe mpenzi,
uloniteka kishenzi,
nyororo ni yako sauti,
itakayo nirejesha nijapokuwa mauti.
© Bradley