...

21 views

MPENDWA MAMA
Ulianza kunipenda,nikiwa bado tumboni
Ukakubali kidonda,ili nije duniani
Hukusita kuwa punda,kuniweka mgongoni
Ahadi ya kunilinda,na kuniweka moyoni
Moyo hukudundadunda,nikikutoka machoni
Nikikosa hunibonda,kwani ipo vitabuni
Mama yangu nakupenda,mwanga nikiwa gizani
© niftyEsther