...

2 views

VIPAJI VYANGU
Mpira naweza cheza, siku nyingi sijacheza,
Shairi la kingereza, kichwani nimewekeza,
Beti nimewekeza, mdomo unaeleza,
Ambacho sijakiweza, ile kujiendeleza.

Nawezaje kutangaza? Mashairi kutangaza! ?
fedga zimeniteleza, google bure nimejaza,
Nafikiri na kuwaza, kuyaimba nakataza,
Acha niite baraza, kitu naweza kusaza.

Nataka kusikiriza, ndoto zangu kutimiza,
Njia za kunihimiza, fedha niweze ingiza,
Yale ya kusisitiza, pia naomba eleza,
Nisije kupitiliza, yakaja kuniumiza.

Sitaki kuendekeza, watu kuwapeleleza,
Kuiga walavyo pweza, ni bora nikajikweza,
Umbea sitouweza, sijibu mkiuliza,
Wakiwa wamendeza, siwezi jipendekeza.

Nikadanganywa na piza, visasi nikalipiza,
Ndoto kuikandamiza, sifa nikazipoteza,
Jera kuniteketeza, nyumba ikawa gereza,
Mama yangu kumliza, kwa nyimbo za Ebeneza.