...

2 views

Moyo wenye kupenda
@Ken Stanley.

Moyo ukisha kupenda, mbona hauambiliki
Ya kipumbavu hutenda, uonye hauonyeki
Ni kama gundi kuganda, ikawa haiganduki
Ah! Moyo wenye kupenda, jama hauambiliki.
Moyo ukisha kupenda, haujui unafiki
Lolote ungautenda, haukosi kuafiki
Haung'amui huenda, watendwa ya kizandiki Ah! Moyo wenye kupenda,huamini unafiki
Moyo ukisha kupenda, la adha hauudhiki
Mpendwa angauponda, bure haubadiliki
Kinyumeche humpenda,huba hazimithiliki
Ah! Moyo wenye kupenda,jamani hauudhiki
Moyo ukisha kupenda, kamwe haujui dhiki
Konda uwe kama ng londa, huba haziteteleki, Hung'ang'ania kupenda, mapenzi hayayumbiki
Ah! Moyo wenye kupenda,hustahimili dhiki
Mtima uliopenda,mbona haueleweki
Ukinaipo kupenda, huwa haudhibitiki
Mabaya uloutenda,hufufuka kwa hamaki
Ah!Moyo wenye kupenda,vipi haueleweki!
@Ken Stanley.
© All Rights Reserved