...

4 views

JINA LANGU
#ShapingIdentities

Salaam hupeana, kabla ya utamburisho,
Jina langu ni Husna, Chikwela jina la mwisho,
Nipende fahamiana, walofanya uanzisho,
Washairi kukutana, kuyafanya maonyesho.

Je walikuwa ni vijana? Au ni wazee sana?
Siku waliokutana, na wakashirikiana,
Ni wapi waliungana? Wazo likapatikana?
Tuambie kwa majina, tuweze fahamiana.

Sifa wazistahili, kuwaenzi wale nguli,
Beti zilitungwa nzuri, kwenye Uhuru wa heri,
Tarehe ya washairi, iwe yetu desturi,
Kwenye hii jamhuri, itengwe ewe waziri.
© Husna Chikwela